
TUGHE KATAVI YATOA HUDUMA YA UCHUNGUZI NA USHAURI WA MAGONJWA
2025-03-08
Katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani, Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Mkoa wa Katavi kiliweka kambi ya Madaktari bingwa kuanzia tarehe 7 hadi 8 Machi 2025 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi. Kambi hiyo ya matibabu ilifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw. Onesmo Buswelu aliyeambatana na Mganga Mkuu wa Mkoa pamoja na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo. Kupitia kambi hiyo TUGHE kwa kushirikiana na Wataalamu walitoa huduma za uchunguzi na ushauri wa magonjwa mbalimbali ikiwemo upimaji wa saratani ya matiti, kansa ya shingo ya kizazi, ushauri wa magonjwa yasiyo ambukiza kwa watu wote, zoezi la kuchangia damu salama, elimu ya homa ya Ini pamoja na upimaji wa virusi vya ukimwi na ushauri nasaha kutoka kwa Madaktari hao.