
TUGHE GEITA WATOA MSAADA WA MAHITAJI MBALIMBALI HOSPITALI YA KATORO, WATUMISHI 12 WAJIUNGA NA TUGHE
2025-03-12
Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Mkoa wa Geita, katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani walitembelea na kutoa msaada kwa Watumishi pamoja na wagonjwa wa Hospitali ya Katoro iliyopo Halmashauri ya Wilaya Geita, ili kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya kutoa huduma hospitalini hapo. Sambamba na hilo TUGHE Mkoa wa Geita walipata pia wasaa wa kutoa elimu kwa Watumishi wa Hospitali hiyo kuhusu umuhimu wa kujiunga na TUGHE ambapo walifanikiwa kusajili wanachama wapya 12. Akizungumza mara baada ya kukabidhi misaada hiyo Mwenyekiti wa TUGHE Mkoa wa Geita, Ndg. Zengo Pole alieleza kufurahishwa na jambo ambalo Kamati ya Wanawake wamefanya kwani itakwenda kuleta hamasa kwa watu wengine kujifunza na kuongeza kuwa Pia itasaidia kuamsha ari kwa Wanawake kujiunga na Chama cha TUGHE.