
TUGHE IRINGA YATOA MSAADA WA BIMA ZA AFYA KWA WAZEE NA KUTEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA NYOLOLO
2025-03-08
Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE ) Mkoa wa Iringa wametembelea na kutoa msaada wa bima za afya 20 kwa Wazee ambazo watazitumia kwa mwaka mzima wa 2025 Sambamba na hilo TUGHE Iringa wametembelea na kutoa msaada wa vyakula na mahitaji muhimu katika Kituo cha Afya Nyololo (Sisi ni kesho) kilichopo Wilayani Mufindi ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na kituo hicho katika kuhakikisha watoto yatima wanapata haki ya malezi bora na elimu. Akizungumza katika maadhimisho hayo Mwenyekiti wa TUGHE Mkoa alieleza kuwa kwa miaka sasa TUGHE imekua na desturi ya kurudisha kwa jamii kila mwaka hususani wakati wanaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika Mkoa wa Iringa yalifanyika jana Machi 8 katika Wilaya ya Mufindi ambapo Mgeni Rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Kheri James ambaye amewataka wanawake kuendelea kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii.