TUGHE MKOA WA SINGIDA WATOA MSAADA KWA WATUMISHI NA WAGONJWA SINGIDA RRH
2026-03-12
Na Mwandishi wetu, SINGIDA Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Singida katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani wametoa msaada wa Vifaa na Mahitaji mbalimbali kwa Watumishi na Wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida. Zawadi zimekabidhiwa na Uongozi wa TUGHE Mkoa kwa kushirikiana na Kamati ya Wanawake TUGHE Mkoa ambapo kwa pamoja wameushukuru Uongozi wa TUGHE Makao Makuu kwa kuwawezesha kufanikisha tukio hilo. Mahitaji yaliyotolewa pamoja na sabuni, mafuta, jagi la Kuchemshia maji na chupa za chai