Tanzania Union of Government and Health Employees

TUGHE MKOA WA KIGOMA WATOA MSAADA WA MAGODORO NA MAHITAJI MBALIMBALI KATIKA HOSPITALI YA WILAYA KAKONKO

2026-03-12

Na Mwandishi Wetu, KIGOMA Tanzania Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania ( TUGHE ) Mkoa wa KIGOMA kikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake Mkoa wa Kigoma, Cde. Angaikundeni John Kweka akiwa sambamba na Mwenyekiti wa TUGHE Mkoa , Cde. Masanja Mchai wamepeleka misaada katika Hospitali ya Wilaya Kakonko iliyopo Mkoa wa Kigoma, kwa kutoa misaada ya mahitaji mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani. Vifaa vilivyotolewa katika hospitali hiyo ni pamoja na Magodoro, Sabuni na Dawa za Meno kwenye Wodi ya Wazazi na Watoto. Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo Mwenyekiti Kamati za Wanawake Mkoa wa Kigoma amesema kuwa wametoa msaada huo ili kuchangia mahitaji ya Hospitali hiyo kisha akahitimisha kwa Kuushukuru Uongozi wa TUGHE Taifa kwa kuwezesha kupatikana kwa Mahitaji na Vifaa hivyo.