Tanzania Union of Government and Health Employees

TUGHE ARUSHA WACHANGIA KUIMARISHA HUDUMA YA AFYA KALOLENI, WATUMISHI 11 WAJIUNGA NA TUGHE

2025-03-07

Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Mkoa wa Arusha, mapema leo Ijumaa tarehe 07 Machi 2025, wametembelea na kutoa misaada ya vitu mbalimbali katika Kituo cha Afya cha Kaloleni kilichopo Jijini Arusha. Zoezi hilo limeongozwa na Makamu Mwenyekiti wa TUGHE Taifa, Dkt. Jane Madete aliyeambatana na Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake TUGHE Taifa, Cde. Catherine Katele, Katibu wa Kamati Wanawake Taifa, Cde. Elizabeth Sarikoki pamoja na Viongozi wa TUGHE Mkoa wa Arusha. Msaada uliotolewa katika Kituo hiko cha Afya ni pamoja na Kompyuta, Viti vya kubebea wagonjwa pamoja na Kitanda lengo likiwa ni kusaidia kuboresha utolewaji wa huduma za Afya Hospitalini hapo. Aidha kupitia tukio hilo Watumishi 11 katika kituo hicho wamefanikiwa kujiunga na TUGHE