Tanzania Union of Government and Health Employees

WAKUU WA IDARA,MAKATIBU WA MIKOA TUGHE WAPATIWA MAFUNZO KUHUSU UHAMASISHAJI

2025-06-20

Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) kikiwa ni moja ya wadau muhimu na Wanachama wa Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Wafanyakazi wa Watumishi wa Umma Duniani (PSI) walishiriki kikamilifu katika mafunzo ya siku tatu kuhusu mbinu mbalimbali za kufanya uhamasishaji wa wanachama utakaoleta tija na ustawi wa Chama cha TUGHE kwa kuongeza idadi ya Wanachama. Mafunzo hayo yaliyondaliwa na PSI kwa kushirikiana na TUGHE yalianza juzi Jumatano tarehe 18 Juni 2025 jijini Dodoma na ambapo yalifunguliwa rasmi na Katibu Mkuu wa TUGHE Cde, Hery Mkunda ambapo yameshirikisha Wakuu wa Idara na Vitengo, Makatibu wa TUGHE Mikoa yote pamoja na Makatibu Wasaidizi.