DKT. MADETE AFANYA ZIARA OFISI YA MKUU WA WILAYA ILEJE
2025-10-15
Makamu Mwenyekiti TUGHE Taifa, Dkt. Jane Madete sambamba na ujumbe wake wakiwa Mkoani Songwe walipata nafasi ya kutembelea katika Tawi la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ileje. Dkt. Madete alikutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya Ileje Mhe. Farida Mgomi kuhusu masuala mbalimbali ya Watumishi. Aidha Makamu Mwenyekiti alipata nafasi ya kutembelea katika Hospital ya Wilaya Itumba ambapo alifanya Uhamasishaji wa Watumishi kwa kuwapatia elimu kuhusu umuhimu wa kujiunga na TUGHE.