MAKAMU MWENYEKITI AKUTANA NA WATUMISHI HOSPITALI YA MJI TUNDUMA
2025-10-15
Makamu Mwenyekiti TUGHE Taifa, Dkt. Jane Madete akiwa katika Siku ya kwanza ya ziara yake tarehe 08/10/2025 Mkoani Songwe alitembelea katika Ofisi ya Mkurugenzi na Hospitali ya Halmashauri ya Mji Tunduma. Akiwa katika maeneo hayo Dkt. Madete alifanikiwa kuzungumza na Watumishi na Wanachama kuhusu masuala mbalimbali ya Kiutumishi ikiwemo umuhimu wa kujiunga na Chama cha TUGHE. Aidha Makamu alipata wasaa wa kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi hao kisha alizichukua na kuhaidi kufanyiwa kazi na zingine zilitolewa ufafanuzi.