UCHAGUZI MKUU TUGHE KATIKA NGAZI MBALIMBALI KUANZA RASMI FEBRUARI 2026 NA KUHITIMISHWA SEPTEMBA 2026
2026-01-16
Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) kinatoa taarifa kwa Wanachama wake wote Nchini kuwa, Chaguzi za ndani ya Chama za kuwapata viongozi wa Chama kwa muda wa miaka mitano ijayo zitafanyika mwaka huu 2026. Chaguzi hizo zitafanyika katika ngazi ya Matawi, Wilaya, Mkoa na Taifa. Kufahamu zaidi kuhusu taarifa hii Soma Gazeti la Mwananchi la Ijumaa Tarehe 16/01/2026 Ukurasa wa 16 Pamoja na Gazeti la Habari Leo la Ijumaa tarehe 16/01/2026 Ukurasa wa 7. Pia tembelea katika Tovuti ya Chama www. tughe.or. tz. Pia waweza kutufuatilja katika mitandao ya Kijamii tunapatikana kwa Jina la TUGHE Tanzania kufahamu zaidi